LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza
MECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa jana Aprili 16, 2026.

Hivyo, timu nne zinazosubiri kuumana katika hatua ya nusu fainali ni Aston Villa, Braga, Nottingham Forest na Freiburg.

Aston Villa ilivuka robo fainali baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Bologna. Villa ilishinda mabao 3-1 katika robo fainali ya kwanza.

Nottingham Forest wakiwa nyumbani jana, waiitandika FC Porto bao 1-0, matokeo yaliyotanguliwa na sare ya bao 1-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Ureno.

Braga wametinga nusu fainali kwa kuifunga Real Betis mabao 4-2 baada ya sare ya bao 1-1 katika robo fainali ya kwanza.

Kwa upande wao, Freiburg walijihakikishia tiketi ya nusu fainali kwa kuifunga Celta Vigo mabao 3-1. Mchezo wa kwanza walishinda mabao 3-0.

Mechi za kwanza hatua ya nusu fainali zitachezwa Aprili 30, 2026, ambapo Villa wataivaa Nottingham, wakati Braga ‘watakiwasha’ na Freiburg.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

BEIRUT, LebanonRAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha...

MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano...

NGONYANI AWAHAMASISHA WATUMISHI MTAMA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPOKEA MWENGE WA UHURU

Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Edwin Ngonyani,...