VENEZUELA YAFUNGULIWA MLANGO NA IMF, BENKI YA DUNIA

Date:

Share post:

CARACAS, Venezuela

SHIRIKA la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia (WB), zimeanza tena uhusiano wa kifedha na Venezuela, hatua itakayoiwezesha nchi hiyo kuanza kupokea msaada kutoka taasisi hizo za kimataifa.

IMF na WB zimeeleza kuwa uamuzi huo umetokana na kuridhishwa na mwelekeo wa uongozi wa sasa chini ya Rais wa mpito, Delcy Rodríguez, pamoja na mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo. 

Hatua hiyo imekuja baada ya takribani miaka saba tangu taasisi hizo zilipositisha ushirikiano na Venezuela mwaka 2019, kufuatia mgogoro wa kisiasa uliosababisha kutokutambuliwa kwa serikali ya wakati huo iliyoongozwa na Nicolás Maduro. 

Wakati huo, IMF na Benki ya Dunia ziliamua kuutambua upande wa upinzani uliokuwa ukiongoza Bunge la nchi hiyo, hali iliyosababisha kusimama kwa misaada na mikopo ya kifedha.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kurejea kwa ushirikiano huo kunatarajiwa kufungua njia kwa tathmini ya uchumi wa Venezuela, uwezekano wa kupata mikopo mipya, pamoja na kusaidia juhudi za kurekebisha deni la taifa hilo. 

Venezuela ni mwanachama wa Benki ya Dunia tangu mwaka 1946, lakini mara ya mwisho kupokea mkopo kutoka taasisi hiyo ilikuwa mwaka 2005.

Imeandaliwa na Hassan Mwacha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

LONDON, UingerezaMECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa...

MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

BEIRUT, LebanonRAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha...

MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano...