MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

Date:

Share post:

BEIRUT, Lebanon
RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha kwa siku 10 vita vilivyokuwa vikiendelea.

Katika taarifa yake, Rais Trump hakuitaja Hezbollah kama sehemu ya mazungumzo, bali Serikali ya Lebabon, ingawa Kundi hilo ndilo linalopigana na Israel kwa wiki sita sasa.

Alichofanya Rais Trump ni kulitaka Kundi hilo kuheshimu hatua ya kusitisha vita, kama ilivyokubaliwa na viongozi wa Israel na Lebanon.

Baada ya Hezbollah kuingia vitani kuisaidia Iran, Israel ilianza kuelekeza mashambulizi yake huko Lebanon liliko Kundi hilo.

Watu zaidi ya 2,100 wameuawa na wengine 7,000 kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, kwa mujibu wa mamlaka za Lebanon.

Je, ni makubaliano yapi yaliyofikiwa hadi vita kusimama kwa siku 10? Miongoni mwa makubaliano ni Israel kuendelea kuwa na haki ya kuchukua tahadhari zote za kujilinda dhidi ya mashambulizi.

Pili, Lebanon inapaswa kupiga hatua muhimu za kuizuia Hezbollah na vikundi vyote vya kigaidi vinavyoishambulia Israel.

Kwamba wanajeshi wa Israel watabaki Kusini mwa Lebanon ili kujihami dhidi ya mashambulizi. Netanyahu amesema: “Tuko pale, hatutoondoka.”

Tatu, pande zote mbili, kwa maana ya Israel na Lebanon, zimeiomba Marekani kuendelea kuratibu mazungumzo ya kusaka suluhu.

Aidha, viongozi wa pande mbili, Netanyahu wa Israel, na Waziri Mkuu wa Lebanon, Nawaf Salam, wameonesha kuvutiwa na hatua hiyo.

Netanyahu amesema mazungumzo hayo ni fursa ya kihistroria ya kusaka amani, wakati Salam anaamini suluhu itakayopatikana itawarejesha maelfu ya raia kwenye makazi yao baada ya wiki sita za kukimbia vita.

Hata hivyo, Hezbollah kutoshiriki mazungumzo hayo kunaacha swali, kwamba Lebabon na Israel zinaweza kumaliza vita pasi na utayari wa Kundi hilo?

Hezbollah waliweza nia yao ya kushiriki mazungumzo na hata kusitisha vita lakini kwa masharti kadhaa, ikiwamo Israel kuondosha wanajeshi wake nchini Lebanon.

Kundi hilo linaungwa mkono na Iran, ambayo nayo ilitaka lijumuhishwe kwenye good mazungumzo yake na Marekani yaliyofanyika Islamabad, Pakistan siku chache zilizopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

LONDON, UingerezaMECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa...

MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano...

NGONYANI AWAHAMASISHA WATUMISHI MTAMA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPOKEA MWENGE WA UHURU

Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Edwin Ngonyani,...