TRUMP AMRUDIA PAPA LEO WA VATICAN

Date:

Share post:

WASHINGTON DC, Marekani
BAADA ya kumtaka kuachana na siasa na badala yake kushughulika na masuala ya Dini, Rais Donald Trump ana ujumbe mwingine kwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV.

Kiongozi hiyo wa Vatican, amekuwa mkosoaji wa utawala wa Marekani, hasa mashambulizi dhidi ya Iran, pamoja na sera za uhamiaji.

Kwa sasa, Rais Trump amesema hana tatizo binafsi na Papa Leo, lakini Kiongozi huyo anapaswa kufahamu uhalifu mkubwa unaofanywa na Israel kabla ya kuikingia kifua.

“Papa anapaswa kuelewa kwamba Iran imeua watu zaidi ya 42,000 kwa kipindi kifupi tu cha miezi ya hivi karibuni,” amesema Trump.

“Walikuwa ni waandamanaji wasio na silaha. Papa anapaswa kujua hilo. Hii ni dunia halisi, siyo ya kufikirika. Papa anaweza kusema kile anachotaka na simzuii lakini sikubaliani naye.”

Kwa upande wake, Papa Leo hajatengua msimamo wake, akisema ataendelea kupaza sauti kulaani vita na kuhimiza amani duniani.

Awali, Papa Leo aliweka wazi kuwa hatishwi na utawala wa Rais Trump aliyesema ushindi wake Vatican ulisukwa ili kuishughulikia Serikali ya Marekani iliyoko madarakani.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

LONDON, UingerezaMECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa...

MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

BEIRUT, LebanonRAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha...

MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano...