MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Date:

Share post:

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT) Taifa, Sheikh Alhaji Musa Salum, aliyemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kumtambulisha uongozi mpya wa JMAT Mkoa wa Mwanza kufuatia mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanyika.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mtanda alisema amepokea kwa furaha mabadiliko hayo, akisisitiza kuwa ni sehemu ya kawaida na muhimu katika uongozi.

Alieleza kuwa mabadiliko husaidia kuleta ufanisi na kuimarisha taasisi.
“Mabadiliko ni sehemu ya maisha ya uongozi. Kama binadamu tunabadilika, tunazeeka na hatimaye tunakufa, hivyo ni muhimu pia kwa taasisi kuwa na mabadiliko ya uongozi,” alisema Mhe. Mtanda.

Aidha, alimpongeza mwenyekiti aliyemaliza muda wake kwa kazi nzuri aliyofanya, huku akiitaka JMAT kuendelea kusimamia na kuimarisha amani kuanzia ndani ya jumuiya hiyo hadi katika jamii kwa ujumla.

pia alisisitiza umuhimu wa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani kutolewa mapema, akiahidi kuchukua hatua stahiki endapo dalili zozote zitabainika.

“Kama kuna dalili zozote za kutoweka kwa amani, naomba mnijulishe. Hiyo ni sehemu ya wajibu wangu kuhakikisha mambo yanaenda sawa,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JMAT Taifa, Sheikh Alhaji Musa Salum, alisema ziara hiyo imelenga kumtambulisha rasmi uongozi mpya wa mkoa huo. Alibainisha kuwa Mwanza ni mkoa mkubwa wenye nafasi muhimu kwa maendeleo ya jumuiya hiyo.

Aliongeza kuwa JMAT inalenga kuimarisha uwepo wake mkoani Mwanza ili kushirikiana kikamilifu na Serikali katika kudumisha amani na kuchochea maendeleo ya kijamii.

Naye Mwenyekiti mpya wa JMAT Mkoa wa Mwanza, Sheikh Mussa Rashid Hassan, aliahidi kuimarisha ushirikiano kati ya jumuiya hiyo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, akisisitiza dhamira ya kuhakikisha JMAT inakuwa na mchango chanya katika maendeleo na ustawi wa mkoa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

LONDON, UingerezaMECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa...

MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

BEIRUT, LebanonRAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha...

NGONYANI AWAHAMASISHA WATUMISHI MTAMA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPOKEA MWENGE WA UHURU

Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Edwin Ngonyani,...