NGONYANI AWAHAMASISHA WATUMISHI MTAMA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPOKEA MWENGE WA UHURU

Date:

Share post:

Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Edwin Ngonyani, amewahamasisha watumishi wa makao makuu kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanayotarajiwa kufanyika Mei 1, 2026 wilayani humo.

Ngonyani ametoa wito huo leo Aprili 17, 2026 wakati akifungua kikao cha watumishi, akisisitiza umuhimu wa tukio hilo la kitaifa na nafasi ya watumishi katika kufanikisha maandalizi yake.

Ameeleza ushiriki wao ni ishara ya uzalendo, mshikamano na kuwajibika kwa jamii wanayoihudumia.

Ameeleza kuwa pamoja na kuhudhuria kwa wingi, watumishi wanapaswa kuonesha nidhamu ya hali ya juu, ikiwemo kuvaa sare maalum (T-shirt) zitakazotumika siku hiyo, pamoja na kuhakikisha huduma katika ofisi zinaanza kutolewa kwa wakati, hasa kuanzia saa 1:30 asubuhi.

Aidha, amewataka watumishi kuendeleza mshikamano miongoni mwao kwa kushirikiana katika nyakati za furaha na changamoto, pamoja na kusaidiana katika kutatua matatizo mbalimbali ya kikazi na kijamii ili kuongeza ufanisi kazini.

Katika kikao hicho, watumishi pia walipata fursa ya kuwasilisha changamoto zao, kutoa maoni na kuuliza maswali, ambapo baadhi ya hoja zilijibiwa papo hapo na nyingine kuahidiwa kufanyiwa kazi na uongozi wa halmashauri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

VIONGOZI LONGIDO WATAKIWA KUHARAKISHA UANZISHAJI WA JUHIZINA

Viongozi wa vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido wametakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mchakato wa kuanzisha...

LIGI YA EUROPA KUMEKUCHA NUSU FAINALI

LONDON, UingerezaMECHI za marudiano hatua ya robo fainali ya msimu huu wa Ligi ya Europa zilimalizika usiku wa...

MAZUNGUMZO YA ISRAEL, LEBANON KUITULIZA HEZBOLLAH?

BEIRUT, LebanonRAIS wa Marekani, Donald Trump, ameutangazia ulimwengu kuwa viongozi wa Israel na Lebanon wameifikia makubaliano ya kusitisha...

MTANDA AKUTANA NA UONGOZI NA JMAT, KUWAASA USHIRIKIANO NA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano...