LONDON, Uingereza
MABOSI wa Real Madrid wanatembea na majina ya makocha wawili, Jurgen Klopp na Mauricio Pochettino, na huenda mmoja wao akaajiriwa kuinoa timu hiyo.
Madrid kwa sasa iko chini ya kocha wa muda, Alvaro Arbeloa, ambaye atamaliza majukumu yake mwishoni mwa msimu huu.
Gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez, anavutiwa na makocha wote, Klopp na Pochettino.
Madrid imeondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na tayari imeachwa pointi tisa na Barcelona iliyojichimbia kileleni mwa msimamo wa La Liga.
Klopp bado yuko nje ya kazi ya ukocha, wakati Pochettino ni kocha wa timu ya Taifa ya Marekani inayojiandaa na fainali zijazo za Kombe la Dunia.
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






