TANAPA YANYACHUKUA TUZO YA DHAHABU KIMATAIFA

Date:

Share post:

MWANDISHI MAALUMU, ARUSHA

MAMLAKA ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), imeshinda tuzo ya dhahabu ya kimataifa ya utoaji huduma bora kwa mwaka 2020 inayotolewa na Taasisi ya European Society for Quality Research (ESQR).

Taarifa ya ushindi huo imetolewa leo na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi – Mawasiliano, Pascal Shelutete ambaye ameeleza kuwa tuzo hiyo itakabidhiwa kwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Jesta Nyamanga, wiki ijayo, jijini Brussels.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kamishna Shelutete ameeleza kuwa TANAPA imeibuka mshindi miongoni mwa washindani 51 kutoka nchi 39 duniani.

“Tuzo za ESQR za huduma bora hutolewa kila mwaka na Shirika la ESQR kwa kutambua taasisi za Serikali na zisizokuwa za kiserikali pamoja na watu binafsi wanaotoa huduma za viwango ya juu. Washindi wa tuzo hii huchaguliwa kwa kuzingatia matokeo ya kura zilizopigwa na taasisi zilizoshinda tuzo hizo awali, maoni ya wateja na utafiti wa masoko.

“Mchakato wa upatikanaji wa washindi wa tuzo hii unajumuisha utafiti wa taarifa mbalimbali kwa umma, machapisho, maoni chanya ya wateja, miradi ya kijamii na vyuo vikuu pamoja na maonyesho,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Kamishna Shelutete.

Anaandika zaidi kuwa tuzo hiyo ni matokeo ya mikakati madhubuti ya TANAPA katika kuhifadhi rasilimali za hifadhi pamoja na mrejesho chanya kutoka kwa wateja wa kitaifa na kimataifa.

“Utambuzi huu utakuwa chachu ya kuendelea kuongeza jitihada za uhifadhi endelevu wa hifadhi zetu na kutangaza vivutio katika masoko mbalimbali na kuendelea kuboresha huduma za utalii,” inasomeka.

Taarifa hiyo inahitimishwa na wito kwa umma, taasisi za kitaifa na kimataifa na wadau wa maendeleo kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhifadhi rasilimali za hifadhi ya Taifa na kuunga mkono juhudi za kukuza utalii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...