MURRO ATAKA MAJI YA BIL 9 NDANI YA SIKU 30

Date:

Share post:

MWANDISHI MAALUMU, ARUMERU

MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji katika Halmashauri ya Arusha kuukamilisha ndani ya siku 30 ili kutotoka nje ya mkataba.

Akizungumza katika eneo linapojengwa tanki kubwa la kuhifadhi maji alikofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi, Murro alisema ameridhishwa na maendeleo yake lakini mkandarasi anapaswa kuhakikisha anaumaliza ndani ya siku 30 zilizosalia kama inavyoelekezwa kwenye mkataba.

Alisema amefanya ziara hiyo baada ya kutokea changamoto ya kupasuka kwa mabomba kila maji yanapofunguliwa kutoka kwenye tanki kubwa lililopo juu, changamoto ambayo imepatiwa ufumbuzi katika ziara hiyo.

“Mradi huu una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tisa na tangu umeanza kutekelezwa sasa tumebakiza siku 30 kwa ajili ya mradi huu kukamilika, lakini nimeona unaenda vizuri ndiyo maana nikasema tutembee ili tuone wapi kuna changamoto ili tuweze kuzitatua kabla ya siku 30 hizi hazijafika tukabidhi mradi.

“Mpaka sasa nataka niwahakikishie zaidi ya asilimia 50 ya maji yameishaingia kwenye mzunguko lakini changamoto kubwa hapa ilikuwa kupasuka kwa mabomba. Ukifungua maji kutoka juu yakishuka mabomba yanapasuka, sasa nikaona hapana lazima nije mwenyewe nijue kwanini yanapasuka. Leo, tumalize ule mzizi wa fitina tujue kwa nini mabomba yanapasuka.

“Sasa tuna habari njema, moja kati ya sababu zilizokuwa zinasababisha mabomba kupasuka ni presha ya maji kutoka juu pale mlimani kwenye tanki kubwa kwa sababu maji yanashuka kwa kasi kwa sababu yakishuka kwa kasi yakikuta wewe hujafungua maji yanajaa yanapasua mabomba, lakini changamoto hii leo tumeimaliza na hamtaiona tena katika maisha yenu. Sasa tunaendelea kuongeza mlazo wa mabomba,” alisema Murro.

Mradi huu mkubwa utahudumia vijiji vitano vilivyo katika Kata ya Ngaramtoni, Lemanyata na Oludonywasi vyenye wakazi zaidi ya 50,000 ambao watanufaika na unatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la Water Aid.

Katika ziara hiyo, Murro aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha, Mbunge wa Arumeru Magharibi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, wawakilishi la Shirika la Water Aid na watendaji wengine wa Serikali na mamlaka za maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...