RAIS TRUMP AMVAA PAPA, AMTAKA AACHE SIASA

Date:

Share post:

WASHINGTON DC, Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameibuka na kauli kali dhidi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, baada ya Papa huyo kukosoa msimamo wa Marekani kuhusu Iran pamoja na sera zake za uhamiaji.

Papa Leo XIV, ambaye ndiye mzaliwa wa kwanza wa Marekani kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ya juu ndani ya Vatican, alieleza wazi kuwa vitisho vya Marekani dhidi ya Iran siyo njia sahihi ya kutatua migogoro, huku akisisitiza kuwa sera za uhamiaji zinazotekelezwa na Marekani hazikubaliki.

Kauli hiyo imeonekana kumkera Rais Trump, ambaye amejibu kwa maneno makali kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Truth Social, akimtaja Papa Leo kama “dhaifu na mhalifu.”

Katika ujumbe wake, Trump amemtaka Papa huyo kuachana na masuala ya siasa na badala yake ajikite katika jukumu lake la kiroho la kuongoza Kanisa Katoliki.

“Leo anapaswa kutekeleza majukumu yake kama Papa, atumie akili… aelekeze nguvu katika majukumu yake ili awe Papa mkubwa, siyo kuwa mwanasiasa,” ameandika Trump.

Hata hivyo, Trump hakukomea hapo, kwani alidai pia kuwa Papa Leo alichaguliwa kushika wadhifa huo kwa lengo la kuushambulia uongozi wake, akionesha kuwa mgogoro wa maneno kati yao unaendelea kuchukua sura ya kisiasa na kidiplomasia.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...