BAADA ya kufungwa bao 1-0 na Sunderland, ni wazi Tottenham inaelekea kushuka Daraja msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Kichapo hicho ni mwendelezo wa hali mbaya waliyonayo, ambayo haijashinda mechi yoyote ya Ligi tangu mwaka 2026 uanze.
Zikiwa zimebaki mechi sita pekee msimu kuisha, Spurs iko juu ya mstari wa kushuka daraja kwa tofauti ya pointi mbili pekee.
Vijana hao wa Kaskazini mwa London wataivaa Brighton wikiendi ijayo, kabla ya kukipiga na Wolves mwishoni mwa mwezi huu.
Je, kocha mpya, Roberto De Zerbi, atainusuru timu hiyo na janga la kushuka daraja?
Imeandaliwa na Hassan Mwasha






