JOHN TERRY AFUATA NYAYO ZA DAVID BECKHAM, ANUNUA KLABU YA COLCHESTER UNITED

Date:

Share post:

LONDON, Uingereza

BEKI na nahodha wa zamani wa klabu ya Chelsea, John Terry, ameinunua klabu ya Colchester United inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini England (EFL).

Terry mwenye umri wa miaka 45 anaingia rasmi kwenye umiliki wa klabu hiyo baada ya kununua hisa zenye thamani ya pauni milioni 14.

Kwa sasa, Colchester United inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo na inaongozwa na kocha Danny Cowley.

Katika kikosi cha timu hiyo pia yupo mpwa wa Terry, Frankie Terry, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Braintree Town.

Awali, Februari 2026, nyota mwingine wa zamani wa Chelsea, Alexandre Pato, alionesha nia ya kuinunua klabu hiyo kabla ya kujiondoa kwenye mchakato huo.

Imeandaliwa na Hassan Mwacha

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...