Historia imeandikwa katika Hospitali ya Mt. Meru ambapo huduma ya Tiba Kemikali (Chemotherapy) imezinduliwa rasmi katika hospitali hiyo.
Uzinduzi huo umefanywa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Jacobo Julius Rombo, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Dkt. Toba Alnason Nguvila, ambapo Hatua hii ni mafanikio makubwa katika kuboresha huduma za matibabu ya saratani, na kuifanya Hospitali ya Mt. Meru kuwa hospitali pekee ya rufaa nchini Tanzania kutoa huduma hiyo.









