Friday, 21 August 2026

MAKONDA ATETA NA  MAAFISA MAENDELEO YA JAMII ARUSHA

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amefanya kikao kazi na Maafisa Maendeleo wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo. Katika kikao hicho kilichofanyika leo Aprili 10, 2026, viongozi hao walijadili kwa kina […]

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amefanya kikao kazi na Maafisa Maendeleo wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu yao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo Aprili 10, 2026, viongozi hao walijadili kwa kina mikakati madhubuti ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha maendeleo katika jiji hilo.

Aidha, kikao hicho kiliweka mkazo mkubwa katika usimamizi na utolewaji wa mikopo ya asilimia kumi isiyo na riba. Mikopo hiyo inalenga kuwainua kiuchumi vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, pamoja na kuchochea maendeleo endelevu ya jamii.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *