Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, leo tarehe 10 Aprili 2026 amefanya kikao kazi na Polisi Kata kutoka wilaya zote za Mkoa wa Tanga.
Kikao hicho kililenga kuimarisha utendaji kazi, kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu na utoaji wa huduma bora kwa wananchi katika ngazi ya kata, pamoja na kusisitiza umuhimu wa nidhamu, uwajibikaji na ushirikiano miongoni mwa askari ili kuendelea kudumisha amani na usalama katika Mkoa wa Tanga.











