ELIMU YA MALEZI DHIDI YA UKATILI WA WATOTO YATOLEWA KIBAHA

Date:

Share post:

MKAGUZI wa Polisi wa Kata ya Picha ya Ndege, Halmashauri ya Mji Kibaha mkoani Pwani, Ibrahim Makaruti, ametoa elimu kwa wazazi kuhusu umuhimu wa malezi bora kwa watoto, akisisitiza kuwa malezi yasiyo sahihi yanaweza kuwa chanzo kikuu cha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Akizungumza na wazazi hao Aprili 10, 2026, Makaruti amesema baadhi ya wazazi wanashindwa kuwalea watoto kwa uangalizi mzuri na kuwajengea maadili mema, hali inayosababisha watoto kukua katika mazingira hatarishi na hivyo kujiingiza katika vitendo vya unyanyasaji, ukatili pamoja na makundi mabaya.

Amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha watoto wanalindwa na wanapatiwa uangalizi wa karibu ili kuzuia matukio ya ukatili.

Aidha, amewahimiza wazazi kuwa karibu na watoto wao kwa kusikiliza changamoto zao na kuwapatia malezi yatakayowajenga kuwa raia wema wa baadaye.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu malezi bora ya watoto ili kudhibiti vitendo vya ukatili, ambavyo vina madhara makubwa kwa watoto na mustakabali wa taifa kwa ujumla.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...