MATONYA AACHIWA KWA DHAMANA KESI YA UBAKAJI NCHINI KENYA

Date:

Share post:

NAIROBI, Kenya

STAA wa Bongo Fleva, Seif Shabani Matonya maarufu kama Matonya, ameachiwa kwa dhamana kufuatia mashitaka ya ubakaji yanayomkabili nchini Kenya.

Msanii huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Jumanne ya wiki hii katika jengo lililopo eneo la Nyali, pwani ya mji wa Mombasa.

Matonya, mwenye umri wa miaka 43, alifikishwa mahakamani mjini Mombasa ambapo alikana mashitaka hayo, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, aliachiwa kwa dhamana baada ya kulipa kiasi cha sh 500,000 za Kenya sawa na sh. milioni 10 huku akitakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani kama sehemu ya masharti ya dhamana.

Matonya alianza kujizolea umaarufu zaidi ya miaka 15 iliyopita, akitambulika kupitia nyimbo zake maarufu kama Vaileti, Anita, Siamini, Taxi Bubu na Mapito.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...