SERIKALI KUENDELEA NA MPANGO WA CHANJO YA HOMA YA INI KWA WATANZANIA

Date:

Share post:

WIZARA ya Afya, imesema inaendelea na maandalizi ya kuweka utaratibu wa kutoa chanjo ya homa ya ini kwa Watanzania wote, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti na hatimaye kutokomeza ugonjwa huo nchini.

Kauli hiyo imetolewa Aprili 10, 2026 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Florence Samizi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Buchosa, Erick Shigongo, aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kutoa chanjo hiyo kwa wananchi wote.

Akijibu kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, Dk. Samizi amesema kwa sasa chanjo ya homa ya ini tayari inatolewa kwa watoto wachanga kama sehemu ya ratiba ya taifa ya chanjo, ambapo hupatiwa muda mfupi baada ya kuzaliwa.

“Chanjo ya homa ya ini inapatikana katika hospitali za Taifa, Kanda, Mikoa pamoja na hospitali zote za Wilaya na Halmashauri. Mwananchi hupimwa kwanza, na endapo hana maambukizi ya virusi vya homa ya ini aina B, hupatiwa chanjo hiyo kwa dozi tatu katika vipindi maalum,” amesema Dk. Samizi.

Amesisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa andiko hilo, Serikali itaanza utekelezaji wa mpango huo ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma hiyo muhimu ya kinga.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...