Friday, 21 August 2026

RAIS WA CUBA AIVIMBIA MAREKANI, AGOMA KUJIUZULU

HAVANA, Cuba RAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, amesema hatojiuzulu kwa sababu ya shinikizo la Serikali ya Marekani. Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu sasa, uhusiano wa Marekani na Cuba umekuwa wa kutilia shaka na wakati fulani Rais Donald Trump alitishia kuivamia kijeshi. Diaz-Canel amesema hatishwi na presha anayopewa na Marekani. “Kujiuzulu siyo sehemu ya misamiati yetu,” […]

HAVANA, Cuba

RAIS wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, amesema hatojiuzulu kwa sababu ya shinikizo la Serikali ya Marekani.

Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu sasa, uhusiano wa Marekani na Cuba umekuwa wa kutilia shaka na wakati fulani Rais Donald Trump alitishia kuivamia kijeshi.

Diaz-Canel amesema hatishwi na presha anayopewa na Marekani. “Kujiuzulu siyo sehemu ya misamiati yetu,” amesema.

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la NBC, amesema Cuba ni nchi huru na inayopaswa kuheshimiwa katika uendeshaji wa mambo yake.
Ameongeza kuwa Kisiwa hicho hakipaswi kuwa koloni la Marekani kwa kusikiliza na kupokea maagizo kutoka kwa Taifa hilo.

“Kwa hapa Cuba, viongozi wanaoingia madarakani huwa hawachaguliwi na Serikali ya Marekani,” amesema.

Imeandaliwa na Hassan Mwasha

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *