Friday, 21 August 2026

CMT YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO KOROGWE

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Korogwe (CMT) imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti ya halmashauri ya korogwe. Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi akishirikiana na wakuu wa idara na vitengo, ikiwa na lengo la kufuatilia maendeleo […]

Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji Korogwe (CMT) imefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo tofauti ya halmashauri ya korogwe.

Ziara hiyo imeongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Bi. Zahara Msangi akishirikiana na wakuu wa idara na vitengo, ikiwa na lengo la kufuatilia maendeleo ya miradi, kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wake.Katika ziara hiyo, CMT ilitembelea miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo elimu na mradi wa maendeleo wa vijana wa mji huo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Bi. Zahara Msangi ametoa wito kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ubora unaotakiwa huku akitoa angalizo kwa wasimamizi hao kusimamia miradi hiyo kwa uweledi ilikuepusha kuisababishia serikali hasara.

Ziara za aina hii zinasaidia kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi kwa wakati

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *