Friday, 21 August 2026

MKE WA TRUMP AKERWA NA SKENDO ZA EPSTEIN

WASHINGTON DC, Marekani MKE wa Rais Donald Trump, Melania Trump, amesema hajawahi kuwa na uhusiano na Jeffrey Epstein, hivyo hataki tena kusikia stori hizo. Melania ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu. Epstein aliyekwishafariki, alikuwa na tuhuma nyingi za udhalilishaji wa kingono, ikisemekana kuwa ndiye aliyewakutanisha Melania na Trump. Hata hivyo, […]

WASHINGTON DC, Marekani

MKE wa Rais Donald Trump, Melania Trump, amesema hajawahi kuwa na uhusiano na Jeffrey Epstein, hivyo hataki tena kusikia stori hizo.

Melania ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu.

Epstein aliyekwishafariki, alikuwa na tuhuma nyingi za udhalilishaji wa kingono, ikisemekana kuwa ndiye aliyewakutanisha Melania na Trump.

Hata hivyo, Melania amekanusha uvumi huo akiuita kuwa ni jitihada za kuharibu heshima na jina lake.

Licha ya kukiri kufahamiana na Epstein, Melania amesema: “Sikuwahi kufahamu chochote kuhusu Epstein kujihusisha na tabia hizo. Sihusiki.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *