SERIKALI YASISITIZA DHAMIRA YAKE KUIMARISHA SEKTA YA FEDHA NCHINI

Date:

Share post:

Serikali imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuimarisha sekta ya fedha nchini ili iwe chachu ya maendeleo ya haraka ya kiuchumi, huku ikisisitiza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wote kwa urahisi na gharama nafuu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), jijini Dar Es Salaam, wakati akifungua Jukwaa la Wadau wa Sekta ya Fedha kwa Mwaka 2026, lenye kauli mbiu isemayo “Sekta ya fedha bunifu na yenye uwajibikaji kwa maendeleo endelevu na jumuishi ya jamii na uchumi.”

Mhe. Balozi Omari (Mb), aliwataka wadau wa sekta hiyo kutumia Jukwaa hilo kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuboresha sera, sheria na mifumo ya kifedha, ili kufikia lengo la kuwa na uchumi imara unaotegemea sekta ya fedha ifikapo mwaka 2050.

“Sekta ya fedha ni mhimili  wa maendeleo ya taifa. Tunahitaji kuhakikisha huduma za kifedha zinawafikia wananchi wote kwa urahisi na kwa gharama nafuu,” alisema, Mhe. Balozi Omar.

Alieleza kuwa Jukwaa hilo lina lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali ili kujadili utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa miaka kumi (2021–2029), huku akibainisha kuwa sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi.

Naye Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), alisisitiza umuhimu wa kudhibiti hatari za kifedha ikiwemo biashara haramu na matumizi mabaya ya mifumo ya fedha, huku akihimiza usimamizi madhubuti wa teknolojia mpya za kifedha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El maamry Mwamba, alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo, ikiwemo kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za fedha, ongezeko la matawi na mawakala wa benki pamoja na ukuaji wa huduma za fedha kidijitali.

Alibainisha kuwa asilimia 76 ya Watanzania sasa wanapata huduma rasmi za kifedha, hatua inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na matumizi ya simu za mkononi na huduma za fedha mtandao.

Washiriki wa jukwaa hilo walipata fursa ya kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta ya fedha, hususan katika maeneo ya ubunifu wa teknolojia, ujumuishwaji wa kifedha na uwekezaji ambapo washiriki hao pia wataendelea na majadiliano mbalimbali.

Jukwaa hilo linatarajiwa kutoa maazimio yatakayosaidia kuimarisha sekta ya fedha na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini, na limewakutanisha wawakilishi wa mabenki, taasisi za bima, vyama vya ushirika pamoja na sekta binafsi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...