UGAIDI WATIKISA UCHAGUZI MKUU BENIN

Date:

Share post:

PORTO-NOVO, Benin

HOFU ya mashambulizi ya kigaidi imeendelea kutanda nchini Benin wakati wananchi wakijiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Aprili 12, 2026.

Raia wa nchi hiyo wanatarajiwa kumchagua rais mpya atakayechukua nafasi ya kiongozi wa sasa, Patrice Talon.

Uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya taharuki, ikiwa ni miezi minne tu tangu jaribio la mapinduzi kutofanikiwa, baadhi ya maofisa wa jeshi walidaiwa kupanga njama za kuipindua Serikali.

Katika hatua za kurejesha hali ya utulivu, Nigeria iliripotiwa kupeleka ndege za kivita kusaidia kudhibiti hali hiyo.

Wakati huo huo, ukanda wa Afrika Magharibi unaendelea kukumbwa na changamoto za kiusalama, huku nchi jirani za Niger, Burkina Faso na Mali zikiwa chini ya tawala za kijeshi.

Hali hiyo imezidisha wasiwasi wa usalama, hasa baada ya kundi la kigaidi lenye uhusiano na Al-Qaeda, JNIM, kufanya shambulizi mwezi uliopita katika kambi ya jeshi na kuua watu 15.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...