TRA UNITED VINARA KADI NYEKUNDU KMC WAKIRUHUSU MABAO MENGI ZAIDI LIGI KUU YA NBC

Date:

Share post:

ZIKIWA zimebaki mechi takribani 12 kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, tayari kadi nyekundu 10 zimeshatolewa katika mechi mbalimbali.

Hata hivyo, takwimu zinaonesha kuwa kati ya kadi nyekundu hizo, matajiri wa soka mjini Tabora, TRA United, wanaongoza kwa idadi kubwa (3).

TRA walikumbana na adhabu hiyo katika mechi dhidi ya Yanga na Simba, ambazo zote zilimalizika kwa suluhu (0-0), na ile waliyotandikwa mabao 2-0 na Mbeya City.

Ukiacha timu hiyo, JKT Tanzania na vigogo wa Chamazi, Azam, nazo zimo kwani kila moja ina kadi nyekundu mbili tangu msimu huu wa Ligi Kuu Bara uanze.

Kwa Azam, wao walipata moja katika mechi dhidi ya Pamba Jiji (2-2) na nyingine dhidi ya Namungo (1-1). JKT ni katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa na walipokutana na Mbeya City (2-2).

Kwa upande wa pili, ukiachana na  Yanga, Azam na Simba, timu 13 zilizobaki zimeonesha kuwa na changamoto kubwa katika safu zao za ulinzi. Kivipi?

Baada ya mechi 18, takwimu zinaonesha kuwa Yanga inaongoza kwa kuruhusu mabao machache (3), ikifuatiwa na Azam (5) na Simba (6), ambayo hata hivyo ina ‘kiporo’ kimoja.

Kinara wa kuruhusu mabao kufikia hatua hii ya msimu ni KMC, ambayo nyavu zake zimeshatikiswa mara 29 katika mechi 18 tu.

Ikifuatiwa na Mbeya City (24), Tanzania Prisons na Fountain Gate (22), Coastal Union (21), Singida Black Stars, Mtibwa Sugar na Namungo (19).

Aidha, zingine kwa mujibu wa takwimu ni TRA United na Namungo (18), JKT Tanzania na Pamba (17), na Mashujaa (16).

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...