WATATU JELA MIEZI 6 KWA KUZUA TAHARUKI YA ‘KUIBIWA NYETI’

Date:

Share post:

WATU watatu wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kila mmoja, baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza taarifa za uongo zilizosababisha taharuki miongoni mwa wananchi kuhusu madai ya kuibiwa nyeti kwa kuguswa begani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 10,2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga amesema uvumi huo ulisababisha vurugu katika baadhi ya maeneo, ambapo watu walishambuliwa, kujeruhiwa na wengine kupoteza mali zao kutokana na hofu iliyozuka.

Amesema Polisi walifanya misako maalum na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 85 wanaohusishwa na tukio hilo. Kati yao, watuhumiwa 16 tayari wamefikishwa mahakamani huku taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 69 zikiendelea kukamilishwa.

Amesema jana watuhumiwa wawili, Onia Bahati Sanga (20) mkazi wa Ntokela na Regan Joshua Kaseke (20) mkazi wa Uyole, walifikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Rungwe kwa kosa hilo walilodaiwa kulifanya kati ya Aprili 5 na 6, 2026 katika eneo la Ntokela.

Mtuhumiwa mwingine, Hashimu William Mwanasenga (29) mkazi wa Mahango, alifikishwa Mahakama ya Mwanzo Ilongo, Wilaya ya Mbarali, kwa kosa alilodaiwa kulitenda Aprili 7, 2026 katika Kijiji cha Mahango.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limetoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kusambaza taarifa za uzushi zinazoweza kuvuruga amani ya jamii na onyo kali kwa watu wanaoandaa na kusambaza maudhui ya uongo kwenye mitandao ya kijamii kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...