ALIYEITUNGUA ARSENAL AWINDWA MAN UNITED

Date:

Share post:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United inampigia hesabu kali kiungo wa Southampton, Shea Charles.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, ndiye aliyefunga bao la ushindi wakati Southampton ilipoifunga Arsenal mabao 2-1 katika mchezo wa hivi karibuni wa robo fainali ya Kombe la FA.

Charles alitua Southampton mwaka 2023 akitokea Manchester City na ameshacheza mechi 67, akifunga mabao manne na ‘asisti’ mbili.

Kiwango chake bora kimezivutia klabu kadhaa, zikiwamo pia Everton na Nottingham Forest, huku thamani yake sokoni ikiwa ni Pauni milioni 20.

Man United inamtolea macho wakati huu ikiwa inajiandaa kumpiga bei Manuel Ugarte, huku kiungo mwingine, Casemiro, naye akiwa njiani kuondoka.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...