Wednesday, 7 October 2026

ATLETICO MADRID YAVUNJA MWIKO CAMP NOU

CATALUNYA, Hispania KWA ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Barcelona, Atletico Madrid ya kocha Diego Simeone imefuta ‘mkosi’ ulioiandama kwa miaka 20. Katika mchezo wa jana Aprili 8, 2026 wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Atletico ikiwa ugenini ilipata mabao yake kupitia Julian Alvarez na Alexander Sorloth. Rekodi zinaonesha kuwa ushindi […]

CATALUNYA, Hispania

KWA ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Barcelona, Atletico Madrid ya kocha Diego Simeone imefuta ‘mkosi’ ulioiandama kwa miaka 20.

Katika mchezo wa jana Aprili 8, 2026 wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Atletico ikiwa ugenini ilipata mabao yake kupitia Julian Alvarez na Alexander Sorloth.

Rekodi zinaonesha kuwa ushindi huo ni wa kwanza kwa Atletico ikiwa Camp Nou tangu mwaka 2006.

Atletico iliposhinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya Barcelona mwaka 2024, mechi hiyo ilichezwa katika Uwanja wa Estadi Olimpic Lluis Companys.

Ni dimba walilokuwa wakitumia Barcelona kwa dharura wakati Camp Nou ikiwa kwenye maboresho.

Katika Uwanja wa Camp Nou, Atletico imepoteza mech zote 25 ilizocheza hapo tangu mwaka 2006.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *