Wednesday, 7 October 2026

DORTMUND YAMPAMBANIA NA SANCHO

MUNICH, Ujerumani KLABU ya Borussia Dortmund inajaribu kumrejesha kiungo wake wa zamani, Jadon Sancho. Sancho aliondoka Dortmund mwaka 2021 na kutua Manchester United kwa ada ya Pauni milioni 73. Mkataba wake unairuhusu Man United kumbakiza hadi mwaka 2027 lakini klabu hiyo ya England haijaonesha kuvutiwa na mpango huo. Mara ya mwisho kwa nyota huyo kuitumikia […]

MUNICH, Ujerumani

KLABU ya Borussia Dortmund inajaribu kumrejesha kiungo wake wa zamani, Jadon Sancho.

Sancho aliondoka Dortmund mwaka 2021 na kutua Manchester United kwa ada ya Pauni milioni 73.

Mkataba wake unairuhusu Man United kumbakiza hadi mwaka 2027 lakini klabu hiyo ya England haijaonesha kuvutiwa na mpango huo.

Mara ya mwisho kwa nyota huyo kuitumikia Man United katika mechi ya mashindano ilikuwa mwaka 2023.

Kwa sasa, Sancho anacheza kwa mkopo Aston Villa lakini Dortmund wanataka arejee Bundesliga mwishoni mwa msimu huu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *