CAIRO, Misri
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amesema yuko tayari kuruhusu Taasisi hiyo kuchunguzwa juu ya tuhuma za rushwa.
Motsepe ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa soka na Serikali nchini Senegal.
Kauli ya Motsepe imekuja baada ya Serikali ya Senegal kuomba ufanyike uchunguzi juu ya vitendo vya rushwa ndani ya Shirikisho hilo.
Ombi la Senegal lilikuja baada ya timu yao ya Taifa kuvuliwa ubingwa wa fainali za AFCON 2025, taji ambalo walikabidhiwa Morocco.
Akizungumza na viongozi wa Shirikisho la Soka la Senegal, pamoja na Rais wa nchi hiyo, Bassirou Diomaye Faye, Motsepe amesema: “Nakaribisha uchunguzi wa rushwa, iwe utafanywa na Serikali au taasisi binafsi.”






