ISRAEL, HAZBOLLAH BADO NGOMA MBICHI

Date:

Share post:

BEIRUT, Lebabon

WAKATI huu Marekani na Iran zikiwa kwenye mapumziko ya wiki mbili ya kusitisha vita, Israel imeendelea kushambulia maeneo mbalimbali ya Lebabon.

Ifahamike kuwa Israel inakwaruzana na Kundi hilo la Lebabon linalohusishwa na vitendo vya ugaidi.

Taarifa zinaeleza kuwa mashambulizi ya jana Aprili 8, 2026 yamelenga maeneo 100 yaliyotajwa kuwa ni kambi za Hezbollah.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Lebanon, mashambulizi hayo yaliyofanyika ndani ya dakika 10 yamegharimu maisha ya watu 182 na kujeruhi wengine 890.

Wizara ya Afya imeeleza kuwa mshambulizi hayo ni makubwa zaidi kuwahi kutokea tangu Israel ilipoanza kuwaandama wapiganaji wa Kundi hilo.

Kwa upande wake, Iran imesema kitendo cha Israel kuendelea kuishambulia Lebanon kinakinzana na hatua iliyofikiwa ya kumaliza vita Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, Rais Donald Trump amejibu kuwa ugomvi wa Israel na Hezbollah hauhusiani na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Iran juu ya kusitisha vita kwa wiki mbili.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...