LOS ANGELES, Marekani
MWANAMKE aliyejulikana kwa jina la Jasveen Sangha amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani baada ya dawa alizompatia Matthew Perry kusababisha kifo cha mwigizaji huyo.
Perry ni staa wa soko la filamu nchini gMarekani (Hollywood) na moja ya kazi zake maarufu ni ‘Friends’.
Alikutwa amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles mwishoni mwa mwaka 2023 na uchunguzi kubaini kuwa alizidiwa na dawa hizo.
Jasveen mwenye umri wa miaka 42, maarufu pia kwa jina la ‘Ketamine Queen’, alikutwa na hatia Septemba, 2025.
Ni baada ya kubainika kuwa alimpatia Perry dawa aina ya ketamine, ambazo mbali ya matumizi mengine, husaidia kupunguza maumivu.
Waendesha Mashitaka wameeleza kuwa nyumba ya bibiye huyo ni ghala la kuhifadhi dawa hizo na amekuwa akiwauzia watu wengi maarufu.







