TRUMP ATISHIA KUWABURUZA CNN MAHAKAMANI KWA KURIPOTI IRAN KASHINDA VITA

Date:

Share post:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amelijia juu Shirika la Utangazaji la CNN akisema limekuwa likizalisha habari za uongo.

Trump hajafurahishwa na namna CNN ilivyoripoti kuwa makubaliano ya Marekani na Iran kusitisha vita kwa wiki mbili ni ushindi kwa Taifa hilo la Kiarabu.

Katika taarifa yake, CNN ilieleza kuwa Iran imeipa masharti kadhaa Marekani na yalipokubaliwa, ndipo ilipoafiki suala ya kusimamisha vita.

Lakini, jambo hilo limepingwa vikali na Trump akisema CNN wamepata taarifa hiyo ya uongo kutoka katika tovuti moja nchini Nigeria.

Hata hivyo, CNN wamekanusha kile alichokisema Trump, kwamba taarifa hiyo imetoka Nigeria, wakisisita kuwa walifanya mahojiano na viongozi wa Iran.

Aidha, amesema mamlaka zinapima athari za taarifa hiyo ya CNN na kama imekiuka sheria, basi hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwamo kufunguliwa mashitaka.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...