Wednesday, 7 October 2026

TMA: MVUA KUBWA DAR NA MIKOA YA PWANI KUENDELEA HADI JUMAPILI

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani kuanzia kesho hadi Jumapili. Mikoa iliyotajwa kuathirika ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro pamoja na Zanzibar. Kwa mujibu wa utabiri wa siku tano uliotolewa Aprili 8,2026 ni kwamba baadhi […]

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani kuanzia kesho hadi Jumapili.

Mikoa iliyotajwa kuathirika ni pamoja na Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro pamoja na Zanzibar.

Kwa mujibu wa utabiri wa siku tano uliotolewa Aprili 8,2026 ni kwamba baadhi ya maeneo katika mikoa hiyo yanatarajiwa kupata mvua kubwa zinazoweza kuleta athari za wastani.

TMA imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari, hususan wale wanaoishi maeneo hatarishi, ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *