Wednesday, 7 October 2026

TYSON FURY ATANGAZA KUMTAKA JOSHUA

LONDON, Uingereza BONDIA wa ngumi za uzito wa juu duniani, Tyson Fury, ameeleza kiu yake ya kuzichapa na Muingereza mwenzake, Anthony Joshua. Fury amesema anatamani kurushiana makonde na Joshua baada ya kumalizana na Arslanbek Makhmudov katika pambano la Aprili 11, 2026. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37, atamvaa Makhmudov wa Urusi na pambano hilo […]

LONDON, Uingereza

BONDIA wa ngumi za uzito wa juu duniani, Tyson Fury, ameeleza kiu yake ya kuzichapa na Muingereza mwenzake, Anthony Joshua.

Fury amesema anatamani kurushiana makonde na Joshua baada ya kumalizana na Arslanbek Makhmudov katika pambano la Aprili 11, 2026.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37, atamvaa Makhmudov wa Urusi na pambano hilo litapigwa katika Uwanja wa Tottenham jijini London.

Ni pambano la kwanza kwa Fury baada ya miezi 16 ya kuwa nje ya ulingo wa ngumi za kulipwa.

Joshua mwenye umri wa miaka 36, hajapigana tangu alipomtandika Jake Paul katika pambano la Desemba, 2025.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *