WATATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA MOTO KATAVI

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Katavi, SACP Kaster Ngonyani amethibitisha vifo vya watu watatu wa familia moja na wengine watatu kujeruhiwa kwa ajali ya moto iliyotokea katika Kijiji cha Ilunde, Kata ya Ilunde, Wilaya ya Mlele mkoani humo.

Kamanda Kaster amesema tukio hilo lilitokea Machi 5, 2026, majira ya saa sita usiku katika Kitongoji cha Miembeni baada ya nyumba hiyo kuungua moto.

Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Winfrida Sheka (32), Peter Lumilija (9) na Thabiza Lumilija (5) wote wakazi wa Kitongoji cha Miembeni.

Amewataja majeruhi watatu kuwa ni Paschal Lumilija (37), Ratifa Lumilija (7) na Elisha Lumilija (1), ambao hali zao zinaendelea vizuri  wakipata Huduma ya matibabu katika kituo cha Afya Ilunde.

Kaster ameeleza chanzo cha moto huo kuwa ni mafuta ya petroli yaliyokuwa yamehifadhiwa ndani ya chumba cha kupikia.

Amesme mafuta hayo yalihifadhiwa na Paschal Lumilija ambaye hujishughulisha na biashara ya kuuza mafuta.

“Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi katika Kituo cha Afya Ilunde kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi,” amesema Kamanda Kaster

Ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari wanapohifadhi vitu vinavyoweza kusababisha milipuko au moto majumbani, akisisitiza kuwa si salama kuhifadhi mafuta ya petroli ndani ya nyumba za kuishi bali yanapaswa kuwekwa katika maeneo maalumu ya kuuzia mafuta.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...