MHARIRI MAKARANGA AFARIKI DUNIA

Date:

Share post:

DAR ES SALAAM

MWANDISHI na Mhariri mkongwe nchini, Revocatus Makaranga amefariki dunia leo Machi 5, 2026 muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa ndugu wa karibu, Makaranga alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye kitengo cha dharura kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, licha ya jitihada za madaktari kumhudumia, alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

Marehemu Makaranga ni mmoja wa waandishi na wahariri wakongwe nchini waliotoa mchango mkubwa katika tasnia ya habari nchini Tanzania.

Makaranga mbali na kufanya kazi katika vyombo vya habari vya umma wakati wa mfumo wa chama kimoja na baadaye vyama vingi, pia alifanya kazi katika kampuni za binafsi za habari za Mwananchi Communications Ltd (MCL), New Habari Ltd.

Makaranga ni mhitimu wa shahada ya uzamili katika uandishi wa habari kutoka Chuo Kikuu cha Cardiff, Wales, Uingereza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...