TUME, MUFTI WATETA MATUKIO YA OKTOBA 29

Date:

Share post:

DAR ES SALAAM

TUME ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, Februari 27, 2026 ilikutana na kiongozi mkuu wa masuala ya sheria ya kiislamu na uongozi wa waislamu Tanzania, Mufti Sheikh Abubakar Zubeir.

Mkutano huo wa Tume na Mufti ulifanyika katika Ukumbi wa Lake Tanganyika uliopo Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jjini hapa.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.

Hivi karibuni, mamlaka ya uteuzi iliiongezea tume muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia Februari 20, 2026 ili iweze kukamilisha uchunguzi wa matukio hayo.

Tume inatakiwa kukamilisha kazi na kuwasilisha taarifa yake kabla au Aprili 3, 2026.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...