KIWANDA CHA KUYEYUSHA CHUPA CHAHATARISHA AFYA ZA WANANCHI

Date:

Share post:

 

Aifang Zhong (Ivan)

 MWANDISHI WA PANORAMA

 MALALAMIKO ya wafanyakazi dhidi ya wawekezaji wa kigeni yanazidi kuongezeka baada ya leo wafanyakazi wa kiwanda cha kuyeyusha chupa za plastiki kilichopo eneo la viwanda. Mbezi Makonde kulalamikia mazingira magumu ya kazi, kunyanyaswa na kufanyishwa kazi bila mikataba ya ajira.

Katika malalamiko hayo, wafanyakazi hao wameeleza kuwa kiwanda hicho kinachafua na kuharibu mazingira kwa kutupa hovyo chupa plaski zinazokusanywa mitaani kwenda kuyeyushwa kiwandani hapo na kwamba mazingira ya kiwanda hicho ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na hakuna mfumo wa kuhifadhi taka na maji yenye kemikali, vinavyotumika katika uyeyushaji.

Wakizungumza kwa ombi la majina yao kuhifadhiwa, walisema  mwajiri wao ambaye ni raia wa China waliyemtaja kwa jina moja la Ivan, anawafanyisha kazi ngumu za uyeyushaji chupa kwa kutumia kemikali bila kuwapa vifaa vya kujikinga (Soksi maalumu za mikononi na viatu vigumu) na amekuwa akiwafukuza kazi bila kufuata sheria za ajira.

“Tuomba na sisi kilio chetu kisikike, tunafanya kazi katika mazingira magumu, kazi yetu hapa ni kuyeyusha chupa, tunatumia kemikali ambazo sisi hatuzifahamu majina lakini hatuna soksi za mikononi wala viatu magumu, tunashika hizo kemikali kwa mikono tu.

“Hatuna vifaa vya kuziba pua na mdomo, wenzetu wanaosafisha chupa nao hawana soksi za mikononi wakati chupa nyingine zinaokotokwa majalalani kabla ya kuja kuyeyusha hapa, wapo wenzetu waliogua kutokana na mazingira magumu ya kazi lakini waliishia kufukuzwa kazi.

“Hatuna mikataba ya kazi  isipokuwa wenzetu wachache ambao nao wanashiriki kutukandamiza kwa sababu wao wapo karibu na hawa wachina na wanalipwa vizuri kidogo, hatuna pensheni, hatupimwi afya zetu. Kiukweli tunafanya kazi hapa kwa sababu hatuna namna nyingine ya kuishi lakini usalama wa afya zetu haupo na wengi tunaambulia magonjwa tu, tunaomba serikali itusikie ije ifanye uchunguzi hapa,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

Aidha walisema bosi wao, Ivan amejijengea uzio wa kutoguswa kwa kujenga urafiki na baadhi ya viongozi wa eneo hilo ambao licha ya kuona chupa zinazookotwa na kupelekekwa kiwandani hapo zikitupwa hadi nje ukuta wa kiwanda na kuziba barabaraba, hakuna hatua zinazochukuliwa.

Alipoulizwa Ivan ambaye uchunguzi umebaini kuwa jina lake halisi ni Aifang Zhong alisema takataka zote nje ya kiwanda chake amekwishaziondoa lakini alishindwa kujibu malalamiko ya wafanyakazi kufanya kazi ngumu zenye kuhatarisha afya zao bila soksi za mikono na viatu vigumu.

Zhong alipobanwa alimpa simu mtu ambaye alikataa kujitambulisha jina na wadhfa wake katika kampuni hiyo ambaye alisema malalamiko yote hayo yana nia ovu na kuomba kuonana na waandishi jambo ambalo Tanzania PANORAMA ililikataa na kusisitiza kupata majibu lakini mzungumzaji huyo hakuwa tayari.

Jitahidi za kumtafuta  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jaffo kuzungumzia uchafuzi wa mazingira katika kiwanda bado zinaendelea.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

EMERY APANGA KUIBOMOA BARCELONA

LONDON, Uingereza KOCHA wa Aston Villa, Unai Emery, anaitaka saini ya beki wa Barcelona, Alejandro Balde, na amewaambia mabosi...

BAYERN YAMKODOLEA MACHO KIUNGO WA TOTTENHAM

LONDON, Uingereza BAYERN Munich inampigia hesabu za karibu kiungo wa Tottenham na timu ya Taifa ya Senegal, Pape Matar...

RIPOTI: IDADI YA WAHAMIAJI ULAYA IMEVUNJA REKODI, UJERUMANI INAONGOZA

LONDON, UingerezaRIPOTI mpya imeonesha kuwa Ulaya nchi za Ulaya zlipokea wahamiaji milioni 64 mwaka 2025, likiwa ni ongezeko...

RAIS WA TAIWAN ASITISHA ZIARA YAKE AFRIKA, CHINA IKITAJWA KUWA CHANZO

TAIPEI, TaiwanRAIS wa Taiwan, Lai Ching-te, ameahirisha ziara yake nchini Eswatini, huku akiitaja China kuwa ndiyo chanzo cha...