![]() |
Mifuko yaviroba |
NA PANORAMA RIPOTA
MFANYANYABIASHA Chun Fang anakwepa kulipa kodi kwa kutumia akaunti yake binafsi kupokea malipo ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda chake na kuuzwa kwa wateja. Tanzania PANORAMA blog imeelezwa.
Habari za uhakika kutoka kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo ambaye ni raia wa China anayemiliki kiwanda cha kutengeneza mifuko inayofahamika zaidi kwa jina la viroba kililichopo Chalinze mkoani Pwani, zimeeleza kuwa anayo ofisi nyingine inayohusika na mauzo eneo Shekilango, jijini Dar es Salaam ambako mipango yake mingi hufanyika.
Akizungumza na Tanzania PANORAMA Blog hivi karibuni, mmoja wafanyakazi wa Fang (jina tunalihifadhi) alisema bosi wake anatumia akaunti zaidi moja kupokea fedha za malipo ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda chake
Alisema akaunti moja ni yake binafsi ambayo huwa anaitumia kupokea malipo makubwa na akaunti nyingine ni ya kampuni ambayo hutumika kupokea malipo kidogo na hiyo hutumika katika masuala yote ya kikodi.
“Hawa jamaa wanatuibia sana, wanaiibia sana Serikali na kila siku wanabuni mbinu mpya za kukwepa kulipa kodi. Inabidi tuisadaie Serikali yetu kuwaanika ili iwabane ipate pesa zake izitumie kwa maslahi mapana ya taifa.
“Huyu mchina mimi ni bosi wangu na nipo naye karibu sana hivyo nina nafasi ya kuona mambo yake mengi yakiwemo ya siri. Yeye ana kiwacha cha kutengeneza mifuko ya viroba, kipo huko Chalinze ila hapa mjini tuna ofisi hapo Shekilango na hapo ndiyo biashara hufanyika.
“Anachokifanya kukwepa kodi ni kwamba ana akaunti mbili, moja ya kwake binafsi na nyingine ya kampuni. Hiyo kampuni naomba msiitaje kwanza jina kwa sasa hilo tunaomba sana kwa sababu huu mchezo mchafu anaufanya yeye na siyo kampuni hivyo haina haja ya kuchafua kampuni bali yeye ndiyo abanwe.
“Sasa ile akaunti yake binafsi huwa inapokea fedha za mauzo ya viroba ambazo ni nyingi na akaunti ya kampuni huwa inaingiziwa fedha za mauzo madogo madogo.
“Ila ana watu maana hata simu anayotumia imesajiliwa na watu wake wanaomlinda hivyo kufanya uchunguzi wa hizi tuhuma zake inabidi ije timu yenye nguvu, isiyoshawishika na.ambayo ina uwezo wa kupambana na wanaomlinda,” alisema mfanyakazi huyo.
Alipoulizwa Fang kupitia simu yake ya kiganjani ambayo inayoonyesha imesajiliwa kwa jina la Calvin Payowela alikataa kuzungumza lolote kisha akakata simu.
Tanzania PANORAMA Blog inaendelea na uchunguzi wa sakata hil