MPANGO MKAKATI WA AMREF WAZINDULIWA

Date:

Share post:

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mpango mkkakati wa miaka nane wa Shirika la AMREF Tanzania na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kufanya ufuatiliaji ili kuhakikisha afua zilizopo katika mpango huo zinatekelezwa kwa ufanisi na kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango huo, Septemba 15, 2023, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam, Majaliwa alisema mpango mkakati huo unaanzia mwaka 2023 hadi 2030 ili kuelekea katika malengo ya maendeleo endelevu ya dunia mwaka 2030.

Alisema mpango mkakati huo unatarajia kugharimu Dola za Marekani milioni 458 kwa miaka yote nane na utajikita katika kuboresha afya ya msingi ikiwemo kutekeleza afua za afya ya uzazi pamoja na afya ya mama na mtoto, afua za magonjwa yasiyoambukiza, kutasaidia kuimarisha afya na ustawi wa Watanzania

 “Niwahakikishie kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Afya Tanzania Bara, Ofisi ya Rais – Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya Zanzibar na wizara nyingine zote ambazo shughuli zenu zinahusiana nazo, itaendelea kushirikiana na AMREF Tanzania kutekeleza mpango mkakati huu,” alisema.

Wakati huo huo, Majaliwa alitoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuzingatia maadili ya nchi wakati wa utekelezaji wa afua mbalimbali.

“Msikubali kutumika kuwa chombo cha kuhamasisha mmomonyoko wa maadili ya Taifa letu. Kila shirika litekeleze majukumu yake kwa kuzingatia mkataba uliopo kati yake na Serikali,” alisema.

Aidha, alizitaka mamlaka za Serikali zinazohusika na usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali kufuatilia kwa karibu utendaji wa mashirika hayo ili kuzuia mianya ya kuhamasisha vitendo vya mmonyoko wa maadili.

Majaliwa alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa kipaumbele Sekta Afya na kutengeneza mazingira rafiki kwa wadau.

“Leo tunaposhuhudia uzinduzi wa mpango huu, haya ni matokeo ya dhamira njema ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan,” alisema.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui ambaye alimuwakilisha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa asasi zisizo za kiserikali za utoaji huduma bora za afya kwa wananchi 

“Tutaendelea kuweka sera na mipango madhubiti ili kufanikisha mpango kazi wenu wa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini,” alisema Mazrui.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa AMREF Tanzania, Dk. Florence Temu alisema gharama za kutekeleza mpango mkakati huo zitakuwa zinaongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2023 zitakuwa ni Dola za Marekani milioni 40.

Alisema kuwa hadi kufikia mwaka 2030, zitahitajika Dola za Marekani milioni 78 hivyo kufanya jumla kuu kuwa Dola za Marekani milioni 458 kwa miaka yote minane ya utekelezaji wa mpango huo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi la Shirika la AMREF Tanzania, Anthony Chamangwana alisema AMREF itaendelea kushirikiana na Serikali ili kuwafikia wananchi kwa wengi kuanzia ngazi ya jamii hadi ngazi ya Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...