MAJALIWA AITAKA TARURA KUWASHIKA MKONO WAHANDISI WAZAWA

Date:

Share post:

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuchukua hatua za makusudi za kuwashirikisha wahandisi wazawa kwenye ujenzi wa miradi nchini.

Agizo hilo alilitoa Septemba 14, 2023 alipomuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya siku wahandisi yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

Alisema kwa kuzingatia utekelezaji wa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano unaolenga kupunguza ukosefu wa ajira kutoka asilimia tisa hadi nane ifikapo 2025/26, Serikali inatarajia kutimiza azma yake ya kuzingatia ushiriki wa Watanzania kwenye sekta ya ujenzi ili kukuza ujuzi. 

“Wizara ya Ujenzi pamoja na bodi ya wahandisi inalifanyia kazi suala la ushiriki mdogo wa wazawa katika miradi ya maendeleo. Hii ni changamoto ambayo mmeiibua, Serikali sasa imeliweka kwenye mpango wa kuhakikisha changamoto hii inafanyiwa kazi ili kuongeza idadi ya wazawa kushiriki katika kazi za ndani,” alisema.

Majaliwa aliesema Serikali imedhamiria kuwawezesha wahandisi wazawa kunufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa  nchini.

“Miradi hii ni fursa kwenu, natoa rai mjipange na muwe na juhudi za makusudi kila mmoja kwenye eneo lake ahakikishe kwa uzalendo alionao na mapenzi kwa nchi yake kuwa kinara katika sekta unayosimamia ili kulijenga taifa letu,” alisema.

Aidha, aliielekeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi iandae mpango mahususi wa kuwaendeleza wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa kwa wingi zaidi wanapohitimu masomo na kusititiza agizo lake hilo litekelezwe kwa ushirikiano na wadau wengine wa uhandisi.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenye alisema Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi katika sekta mbalimbali za kiuchumi kupitia uanzishaji wa viwanda, uendelezaji wa miundombinu ya kilimo, nishati, maji, uvuvi, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano

“Mwaka 2023/2024, Serikali imetenga miradi maalumu ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa ajili ya wakandarasi wanawake ambao zabuni zitashindanishwa kwa wakandarasi wanawake tu,” alisema. 

Kwa upamde wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Menye David Manga alisema bodi inatarajia kufanya mageuzi ya teknolojia ili kuhakikisha wahandisi waliosajiliwa na wenye sifa wanakuwepo wa kutosha kwa ajili miradi mbalimbali nchini ili kujenga dhana halisi ya ushirikishwaji wa wazawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...