UJIO WA ASA NA NGOMA MPYA 'OCEAN'

Date:

Share post:

Mwanamuziki Asa


JOSEPH SHALUWA

MWANAMUZIKI mahiri kutoka nchini Nigeria, Asa ameachia ngoma yake mpya iitwayo Ocean aliyofanya na prodyuza maarufu, Priime, ikiwa ni maandalizi ya kutoa albamu yake ya V (Five) inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Kuachiwa kwa ngoma hiyo, kunakuja muda mfupi baada ya mwanadada huyo, kutoa ngoma nyingine, Mayana ambayo imepokelewa vyema na mashabiki wa muziki ndani na nje ya mipaka ya Nigeria.

Dairekta mkali, Meji Alabi ndiye aliyefanya video ya wimbo huo ambapo kwa kuzingatia mashairi na staili ya uimbaji ya Asa, ukichanganya na vionjo alivyoviweka dairekta huyo katika video hiyo iliyopo katika mfumo wa ‘visuals’, kwa pamoja vimeifanya video hiyo kuwa moto wa kuotea mbali.

Akiuzungumzia wimbo huo, Asa amenukuliwa akisema: “Ocean ni miongoni mwa kazi bora kabisa katika tasnia ya muziki. Nguvu za kujua mimi ni nani, nini nakitaka, kufanya ninachokitaka na kuishi maisha ya ukamilifu kama Mungu alivyoniumba.”

Ocean ni miongoni mwa ngoma zilizopo kwenye albamu ya V (Five) ya mwanadada huyo inayotarajiwa kuingia mitaani Februari 25 na ilitengenezwa dakika za mwisho kabla mwanadada huyo hajaamua kurudi Nigeria baada ya ziara za kimataifa za muziki, kuahirishwa kutokana na janga la Corona.

Pia mwanadada huyo anatarajia kufanya shoo jijini London, Uingereza Mei 3, 2022 katika Ukumbi wa Royal Albert Hall, ikiwa ni mwendelezo wa kuutangaza muziki wake kimataifa.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...