MACHOZI YA BURIANI YA DK. AKINWUMI KABURINI KWA HAYATI RAIS DK. MAGUFULI

Date:

Share post:

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Akinwumi Adesina akisali katika Kaburi la Rais wa Awamu wa Tano, Hayati Dk. John Pombe Magufuli, lilipo Chato mkoani Geita

  

RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

IKIWA ni takribani mwaka mmoja sasa tangu aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Hayati Dk. John Pombe Magufuli azikwe kaburini kijijini Chato, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Akinwumi Adesina amefika katika kaburi hilo na kudondosha machozi ya buriani.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Akinwumi Adesina

 

Dk. Akinwumi ambaye alisafiri kutoka Abidjan , Ivory Coast yaliko Makao Makuu ya AfDB, aliwasili Mkoa wa Geita siku chache zilizopita na kwenda moja kwa moja Kijiji cha Chato, mahali alikozikwa Hayati Rais Dk. Magufuli ambako alipiga magoti na kumuombea mapumziko mema.

Safari yake kuja hapa nchini ilikuwa na baraka za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimpatia kibali cha kuja kuhani msiba wa Hayati Dk. Rais Magufuli na katika shukrani alizozitoa baada ya kuhani, alisema; “Ninamshukuru Rais Samia kunipa kibali cha kuja kuhani msiba wa Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

 

Akimzungumzia Hayati Rais Dk. Magufuli, alisema alikuwa mwanamajumui wa Afrika wa kizazi cha sasa mwenye kariba  ya wanamajumui wa Afrika wa kizazi kilichopita.

Hayati Rais Dk. John Pombr Joseph Magufuli

 

Akiwataja wanamajumui wa Afrika wa kizazi kilichopita aliowafananisha na Hayati Rais Dk. Magufuli, alianza na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Waziri Mkuu wa Kwanza na Rais wa Ghana, Hayati Kwame Nkrumah, Waziri Mkuu wa Kwanza wa DRC, Hayati Patrice Lumumba na Rais Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Kenya, Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Raus wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

 

Wengine aliowataja ni Rais wa Kwanza wa Nigeria, Hayati Nnamdi Benjamin Azikiwe, Rais wa zamani wa Burkina Faso, Hayati Thomas Isidore Noel Sankara, Rais wa Kwanza wa Zambia, Hayati Kenneth David Kaunda, aliyekuwa Rais wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Hayati Oliver Reginald Kaizana Tambo.

Katika orodha hiyo ndefu ya wanamajumui wa Afrika aliyoitaja akiwalinganisha na Hayati Rais Dk. Magufuli ni pamoja na mwanaharakati na mwanahistoria wa Amerika, Hayati William Edward Burghardt Du Bois, mwanaharakati na mwanahabari wa Jamaica, Hayati Marcus Mosiah Garvey, Waziri Mkuu wa Kwanza na Rais wa Zimbabwe, Hayati Robert Gabriel Mugabe, Hayati Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia na Rais wa Kwanza Mwafrika wa Afrika ya Kusini, Hayati Nelson RolihlahlaMandela.

Dk. Akinwumi alieleza zaidi kuwa Hayati Rais Dk. Magufuli alikuwa mbeba maono, kiongozi imara na mwanamapinduzi aliyeipa Afrika taswira mpya katika kipindi chake kifupi cha uongozi na kwamba viongozi wa aina yake hawazaliwi mara kwa mara

Aidha, Dk. Akinwumi alisema Hayati Rais Dk. Magufuli alikuwa alama ya maendeleo na uzalendo na kwamba wakati wa uhai na utawala wake, aliushangaza ulimwengu kwa hatua za haraka za kimaendeleo ambazo Serikali aliyokuwa akiiongoza ilizisimamia na hasa ujenzi wa miundombinu ya umeme, barabara, maji, afya na elimu na pia kuiwezesha Tanzania kuingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati.

Mwanaharakati na mwanahistoria wa Amerika, Hayati William Edward Burghardt Du Bois

Mwanahabari wa Jamaica, Hayati Marcus Mosiah Garvey .

Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia .

Rais Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Kenya, Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Rais wa Kwanza wa Zambia, Hayati Kenneth David Kaunda.

Waziri Mkuu wa Kwanza na Rais wa Ghana, Hayati Kwame Nkrumah.


 
 
 
Rais wa Kwanza Mwafrika wa Afrika ya Kusini, Hayati Nelson RolihlahlaMandela.

Waziri Mkuu wa Kwanza na Rais wa Zimbabwe, Hayati Robert Gabriel Mugabe.


 
Rais wa Kwanza wa Nigeria, Hayati Nnamdi Benjamin Azikiwe.


 
Aliyekuwa Rais wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini, Hayati Oliver Reginald Kaizana Tambo

Waziri Mkuu wa Kwanza wa DRC, Hayati Patrice Lumumba.


 
Rais wa zamani wa Burkina Faso, Hayati Thomas Isidore Noel Sankara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...