RONALDO ATUA AL NASSR

Date:

Share post:

RIPOTA PANORAMA

NAHODHA wa Timu ya Soka ya Ureno, Cristian Ronaldo amesajiliwa na timu ya Al Nassr ya Saudi Arabia ambako atakuwa anaweka kibindoni kitita cha Euro milioni 117 kwa mwaka.

Taarifa zilizopatikana mapema leo kutoka vyanzo mbalimbali vya habari vya nchini Saudi Arabia zimeeleza kuwa Ronaldo amejiunga na klabu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ambao utadumu hadi mwaka 2025.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 sasa, amejiunga na Klabu ya Al Nassr akitokea Klabu ya Manchester United ya Uingereza ambayo aliikosoa vikali na kuishutumu kwa kumsaliti muda mfupi kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la 2022 lililofanyia nchini Qatar.

Baada ya kusaini mkataba wa kucheza Klabu ya Al Nassr, Ronaldo amekaririwa akieleza kuwa anatamani kupata uzoefu wa ligi mpya ya soka katika nchi tofauti.

Amesema anayo bahati ya kushinda kila kitu alichokidhamiria kaktika maisha yake ya soka barani Ulaya na kwamba anahisi sasa ni wakati mwafaka kwake kubadilisha uzoefu wake kisoka akiwa katika Bara la Asia.

Timu ya Al Nassr ni mabingwa mara tisa wa ligi ya nchini Saudi Arabia na wameeleza kuwa usajili wao kwa Robaldo ni wa kihisitoria kwani utahamasisha ligi ya nchini humo, taifa na vizazi vijavyo kuwa bora zaidi kisoka.

Wakati wa msimu wa joto, Ronaldo alikataa mkataba wa Euro milioni 315 kwa mwaka wa kujiunga na Timu ya Al Hilal ya Saudi Arabia kwa kile alichoeleza kuwa ameridhika kusalia Manchester United.   

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...