Monday, December 23, 2024
spot_img

MAJALIWA ATAKA KUANZISHWA MAJUKWAA YA KIUCHUMI

RIPOTA WA WAZIRI MKUU

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi na watumishi wa balozi za Tanzania nje ya nchi kuendelea kufanya tathmini ya fursa za kiuchumi ambazo nchi inaweza kupata kutokana na ushirikiano wa kidiplomasia katika nchi walizopo.

Akizungumza jana na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini uliopo katika Jiji la Pretoria, alisema ni vema balozi hizo zikaanzisha majukwaa ya kiuchumi yatakayowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi hizo katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo ardhi, madini, utalii, mawasiliano na biashara.

“Muwasihi wafanyabiashara na wawekezaji waje kuwekeza Tanzania na washirikiane na Watanzania kufungua makampuni, hii itatusaidia Watanzania kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha biashara,” alisema Majaliwa.

Alisema watumishi wa balozi za Tanzania hawana budi kuandaa makubaliano baina ya Tanzania na nchi walizoko ambayo yataonyesha nini kinatakiwa nchini humo na ambacho kinapatikana kwa wingi Tanzania.

“Hapa kwenu, ubalozi unapaswa kutengeneza makubaliano maalumu ya kibiashara miongoni mwa nchi hizi mbili na kubainisha aina ya bidhaa ambazo zinapatikana Tanzania kwa wingi na zinahitajika Afrika Kusini,” alisisitiza.

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ubalozi wa Pretoria unapaswa kuendelea kuhamasisha watalii kutoka nchini humo kwa kubainisha vivituo vya utalii vilivyoko Tanzania ambavyo nchi hiyo haina huku akitolea mfano Mlima Kilimanjaro.

Awali, akitoa taarifa ya kiutendaji ya ubalozi huo, Kaimu Balozi Peter Shija alisema Tanzania inaweza kunufaika zaidi na fursa za biashara zilizopo nchini humo kwa kuuza mazao kama, mchele, maharage, korosho na mazao ya matunda.

Nyingine Zinazohusiana na Hii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Tufuatilie

0FansLike
3,913FollowersFollow
0SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Habari Nyingine Mpya