NILIONDOKA TOC KULINDA HESHIMA YANGU NA YA TAALUMA YANGU

Date:

Share post:


RIPOTA PANORAMA

0711 46 49 84

ALIYEKUWA Mweka Hazina wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Charles Nyange amesema aliacha kazi katika kamati hiyo kwa sababu ya kulinda heshima yake na heshima ya taaluma yake.

Nyange ameyasema hayo leo alipozungumza na Tanzania PANORAMA Blog iliyomuuliza sababu zilizomuondoa kwenye utumishi wake huo na iwapo katika kipindi cha utumishi wake ndani ya TOC alipata kukutana na vikwazo vya aina yoyote katika utendaji wake.

Katika majibu yake mafupi, Nyange alisema yeye ni mhasibu kitaaluma hivyo aliamua kuacha kazi kwa hiari yake kwa sababu wanataaluma wenzake wangamshangaa lakini hakuwa tayari kufafanua zaidi wangemshangaa kwa sababu zipi.

“Niliondoka mwenyewe, niliamua kuacha hiyo kazi mimi mwenyewe. Nina muda mrefu sipo pale hivyo siwezi kuyazungumzia sana mambo ya hapo. Mimi ni mhasibu kitaalumu hivyo wahasibu wenzangu wangenishangaa sana….”

“Nimefanya kazi TOC kwa zaidi ya miaka minne na nilikuwa najitolea lakini niliamua kuacha kazi kwa sababu ya kulinda heshima yangu na heshima ya taaluma yangu. Lakini TOC inaendeshwa kwa fedha kutoka IOC, sasa hayo mengine waulizeni wenyewe, muulizeni Katibu Mkuu kwa sababu mimi vitabu vyote niliacha hapo,” alisema Nyange.

Kauli hii Nyange imekuja siku chache baada ya Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi kufanya mahojiano na PANORAMA kuhusu kuandamwa na tuhuma za ufisadi wa fedha zinazotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ambapo alieleza kuwa tuhuma hizo zinatolewa na watu wenye lengo la kumchafua.

Hata hivyo, Bayi alikataa kujibu maswali mengine aliyoulizwa na PANORAMA alipokutana nayo kwa mara ya pili ofisini kwake Kibaha akiwa na Makamu Mwenyekiti wa TOC, Henry Tandau, waandishi wa habari wawili ambao ni wapambe wake pamoja na watu wengine kadhaa.

Ilielezwa kwamba maswali yote aliyoulizwa Bayi yatajibiwa katika mkutano wa waandishi wa habari utakaotishwa mahususi kwa ajili ya kujisafisha.

 

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

USIYOYAJUA KUHUSU KOCHA ALIYEANDIKA HISTORIA BUNDESLIGA

MUNICH, Ujerumani JINA la Marie-Louise Eta limeandika historia katika soka la Ujerumani baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa...

BURNA BOY HATAKI MAZOEA, ‘BIFU’ KWAKE KAWAIDA TU

HIVI karibuni, supastaa wa muziki wa Afrobeat, Burna Boy, aliingia kwenye mikono ya Chama cha 'Ma-dj' nchini Nigeria,...

BURKINA FASO IKO HOI AU HAI CHINI YA KAPTENI TRAORE?

HATUA ya kutangaza kuwa raia wake waaitarajie demokrasia imeibua maswali mengi juu ya uongozi wa Kapteni Ibrahim Traore...

SIMU YAKO CHANZO CHA UGONJWA WA MOYO, SARATANI?

UKWELI ulio wazi ni kwamba matumizi ya simu za mkononi yameongezeka kwa kasi duniani, Tanzania ikiwa na 'laini'...