SIRRO, MONGELLA WATOA RAI LOLIONDO

Date:

Share post:

IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa Loliondo mapema wiki hii

 MWANDISHI WETU

LOLIONDO

MKUU wa Jeshi la Polisi, (IGP) Simon Sirro  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC) John Mongella wamefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro  kukagua kazi ya kuweka alama za mipaka.

Viongozi hao walifanya ziara hiyo mapema wiki hii na kueleza kuwa wameridhishwa na mwenendo wa kazi wa kuweka alama hizo za mipaka.

Akizungumza baada ya ukaguzi, IGP Sirro awalitaka wataalamun wanaofanya kazi hiyo kujituma ili ikamilike kwa wakati.

Aidha Sirro alitoa rai kwa wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na Serikali kwa sababu la kuweka mipaka hiyo ni kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.

‘Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote  na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema kama taifa’, alisema IGP Sirro.

Kwa upande wake RC Mongella alimhakikishia IGP Sirro kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha imejipanga kuhakikisha kuwa kazi inaendeshwa kwa hali ya utulivu na kwa kuzingatia sheria za nchi.

MATUKIO MENGINE KATIKA PICHA IGP SIRRO NA RC MONGELLA WALIPOZURU LOLIONDO


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...