MGANGA WA KIENYEJI ADAIWA KUMFILISI MFANYABIASHARA MWANZA

Date:

Share post:

Gari la kifahali aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa likimilikiwa na mfanyabiashara Remoy Kibombe aliloliuliza ili kupata fedha za kwenda kumpa mganga wa kienyeji

 

MWANDISHI WETU

MFANYABIASHARA Remoy Kibombe wa jijini Mwanza amefilisika baada ya kuuza mali zake zote kwa ajili ya kukidhi matakwa ya mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la Salim Kanyani ya kupata utajili.

Akizungumza na Tanzania Panorama hivi karibuni, Kibombe alisema alifikia uamuzi wa kuuza mali zake zote kwa maelekezo ya mganga Kanyani, aliyemtaka ampatie fedha kiasi cha Shilingi bilioni moja ili azifanyie dawa ziongezeke zaidi ya maradufu.

Alisema alishawishika na kauli za mganga huyo baada ya kumfanyia muujiza wa kwanza ambapo alimpatia fedha za kigeni (Dola za Marekani) 15,000 ambazo alizifanyia dawa zikaongezeka maradufu.

“Huyu mganga nilimjua baada ya kwenda kutafuta tiba ya maradhi yaliyokuwa yakinisumbua na nilielekezwa na jamaa yangu, nilipofika kweli alinihudumia na tukiwa katika maongezi nilimwambia mimi ni mfanyabiashara.

“Akaanza kunishawishi kuwa yeye anazo pia dawa za kuongeza utajili kwa sababu anayo miungu yake ambayo akiiomba ina uwezo wa kuongeza kiasi fedha zinazofanyiwa maombi kikawa maradufu.

“Awali niliamua kumjaribu, nikampatia kiasi fulani cha fedha ambazo ni Dola za Marekani 15,000, kweli akazifanyia hiyo miujiza yake akaniletea Dola za Marekani 30,000. 

Nikaona anaweza kuwa anasema kweli. Nikataka nimpelekee kiasi kingine lakini siyo kingi akakataa akasema hiyo miungu yake imeelekeza sasa nitoe Shilingi bilioni moja ndiyo itafanya miujiza ya kuziongeza ili ziwe bilioni mbili,” alisema.

Akielezea zaidi alisema baada ya kuuza mali zake hizo na kupata fedha, hazikufika Shilingi bilioni moja hivyo alichukua fedha alizokuwanazo benki ili kufikisha Shilingi bilioni moja alizokuwa ametakiwa na mganga kisha akampelekea lakini baada ya kumpatia alianza kumzungusha akimtaka awe na subira wakati miungu yake akishughulika kuziongeza fedha hizo lakini baada ya muda mrefu kupita alibaini kuwa ametapeliwa.

Alisema amekwishalifikisha suala hilo katika vyombo vya ulinzi na usalama bila kufafanua zaidi lakini hadi sasa hajapata majibu kuhusu malalamiko yake hayo.

Alipotafutwa Kanyani ili kuzungumzia madai hayo dhidi yake alisema yeye hajawahi kushtakiwa mahal ipopote kwa makosa ya kuwatapeli wateja wake na alikiri kuwa anajihusisha na uganga wa kienyeji.

Tanzania PANORAMA inaendeleanauchunguziwasakatahili.

 


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

SOMA HIYO! ISRAEL NDIYO WAASISI WA MIKWAJU YA PENALTI

LONDON, Uingereza NI jioni ya Agosti 5, 1970 kwenye Uwanja wa Boothferry Park mjini Hull, Manchester United ikiwa ugenini...

AMEJIPATA! LAMPARD ALIVYOREJEA EPL AKIWEKA REKODI

LONDON, Uingereza IKIWA ni miezi 18 tu imepita tangu alipoajiriwa, Frank Lampard ameiwezesha Coventry City kupanda daraja na kurejea...

USICHUKULIE POA! PATORANKING ALIUZA SUMU YA PANYA MITAANI KABLA YA ‘KUTOBOA’

LAGOS, Nigeria WAHENGA walisema maisha ni safari yenye milima na mabonde. Kwamba katika kuishi kwako, si nyakati zote zitakuwa...

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...