TANZANIA INA WATU THABITI AFRIKA- DK ABBAS

Date:

Share post:

 

 

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbas emesema watanzania ni watu thabiti  ba webte historia ya kutukuka katika mapambano ya ukombozi wa Bara la Afrika.

Dk Abbas ameyasema hayo jana alipotembelea makao makuu ya ofisi za Ukombozi wa Bara la Afrika kujionea changamoto zinazoukabili.

Akizungumza katika ofisi hizo, alisema Tanzania ni nchi yenye watu wenye historia thabiti barani Afrika kutokana na kushiriki kikamilifu kuzikomboa nchi nyingi barani Afrika.

“Tanzania si tu imetoa mchango mkubwa katika historia ya Ukombozi wa Afrika bali imegharamika mno kuanzia watu wetu, fedha zetu na hata kuiweka nchi yetu katika hatari ya kushambuliwa.

“Viongozi wetu walifanya uthubutu mkubwa na sisi leo sio watu poa, tuko imara kuilinda nchi yetu na sisi tuliopewa dhamana ya mradi huu lazima tutimize wajibu wetu ili kuitunza historia hii na kuwajengea vijana wa sasa uzalendo na utamaduni wa kuwa watu wa kuthubutu kwa ajili ya nchi yao na Afrika,” alisema Dk. Abbas.


 

Alisema kutokana na umuhuimu wa ofisi hizo ambazo Umoja wa Afrika (AU) uliamua makao makuu yake yawe Dar es Salaam na serikali imeuweka chini ya usimamizi wa Idara ya Utamaduni katika wizara ya Habari sasa unahamishwa kutoka Idara ya Utamaduni na kuwa moja kwa moja chini ya Ofisi yake.

“Tunataka kwenda kasi na kwa viwango, wazee wetu walithubutu kufanya mambo makubwa kutufikisha hapa tulipo, sasa naona mnafanya kazi kubwa lakini mradi huu bado unachangamoto nyingi ambazo Idara ya Utamaduni pekee haiwezi kuzipeleka kwa kasi, watabaki washauri wa kitaalamu tu kwangu na kwa mradi huu, lakini kuanzia leo 7, Disemba, 2020, mratibu wa mradi huu atawajibika na kuripoti moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,” aliagiza Dk. Abbas.

About The Author

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

UCHUMI WA CHINA WAZIDI KUIMARIKA

BEIJING, China LICHA ya vita vya Marekani na Iran kuonekana kuitikisa dunia, China imeendelea kupiga hatua kubwa katika eneo...

SIKU 100 ZA RAIS MPYA WA VENEZUELA: MABADILIKO NA MASWALI MAPYA

CARACAS, Venezuela BAADA ya vikosi vya Marekani kumng’oa madarakani aliyekuwa Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro kwenye oparesheni ya Januari...

MAELFU YA FAMILIA SUDAN BADO WAKIMBIA VITA, HALI YA MAISHA YAZIDI KUWA MBAYA

MAELFU ya familia nchini Sudan bado wanalazimika kuyakimbia makazi yao, miji na hata mipaka ya nchi kufuatia vita...

ISRAEL YAENDELEA NA OPERESHEN DHIDI YA HEZBOLLAH NCHINI LEBANON

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jeshi la nchi yake linaendelea na operesheni dhidi ya wanamgambo wanaoungwa...