Watatu Chadema kortini

Date:

Share post:

Watatu Chadema kortini

DAR ES SALAAM

 
 
Watu watatu waliokuwa wakishikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, jana walifikishwa kortini wakituhumiwa kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Watuhumiwa hao ambao wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa.
Walisomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, aliyeieleza mahakama wanaunganishwa na wenzao 28 walioshtakiwa wiki iliyopita.
Wakili Mwita alidai mahakamani kuwa washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali maeneo ya Mkwajuni, Kinondoni mwezi uliopita.
Kwamba walitenda kosa hilo, Februari 16,
kinyume cha sheria wakiwa na nia ya kufanya uvunjifu wa amani na kusababisha taharuki, hata hivyo , walikana shtaka hilo.
Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi haujakamilika hivyo kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine na Hakimu Mwambapa, alitoa masharti ya dhamana kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 1.5. Washtakiwa wote walipata dhamana. 
Kesi hiyo itatajwa Machi 8, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

KIFO CHA BOSI KINAVYOITESA LEICESTER CITY

LONDON, UingerezaMIAKA 10 iliyopita, Leicester City waliishangaza dunia walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) mbele ya...

ISHU YA RASHFORD BADO PASUA KICHWA

MANCHESTER, UingerezaKOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema bado haijafahamika kama Marcus Rashford atarudi klabuni hapo au atabaki...

BARCA YAPATA MRITHI WA LEWANDOWSKI

CATALUNYA, HispaniaKLABU ya Barcelona imeanza mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kati wa Real Mallorca, Vedat Muriqi, ikiamini anatosha...

ARSENAL AKILI YOTE KWA MONGA

LONDON, UingerezaARSENAL ya Kaskazini mwa Jiji la London imeonesha nia ya kumsajili winga anayefanya vizuri Ligi Daraja la...